Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Kocha wa Simba, Pierre Lechantre amesema ugumu wa mechi wanazokutana nazo kwa sasa ndiyo sababu kubwa inayomfanya kutowatumia kabisa Haruna Niyonzima na Said Ndemla katika mechi mbili zilizopita.
Niyonzima ambaye hivi karibuni alitoka katika kipindi cha majeraha, hajawa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kimecheza dhidi ya Prisons na kushinda mabao 2-0 na dhidi ya Mbeya City waliyoshinda kwa mabao 3-1. Mechi zote zilichezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
HABARI MPYA JAGWANI BAADA YA USHINDI BOFYA KUISOMA>>>>
Lechantre amesema ameshindwa kuwatumia viungo hao kwenye mechi hizo mbili kwani wapinzani wao walikuwa wanakaba sana na kutumia nguvu nyingi.
“Kuhusu Niyonzima kutocheza nilifanya hivyo kwa sababu kwenye mechi hizi mbili ambazo tumecheza na Mbeya City na Prisons, nilibaini kwamba wapinzani wangu wana watu ambao wanacheza kwa nguvu kubwa sana.
“Pia watu wao wanakaba sana hivyo nikaona nisiwatumie viungo halisi wanaocheza nafasi ya kiungo mchezeshaji na nikawapanga watu wengine.
“Kama mechi na Prisons utaona kabisa wapinzani wetu walikuwa wanacheza kwa kukaba mtu na mtu, sasa hapo ningesema kwamba nitumie viungo wachezeshaji ambao kwenye suala la kukaba siyo wazuri ingekuwa pigo kwetu hivyo nilichofanya ni kuwaweka pembeni tu.
“Lakini kwenye michezo ijayo wanaweza kutumika kwani siyo kila mchezo ambao tutacheza mambo yatakuwa hivihivi,” alisema Lechantre raia wa Ufaransa.
CHANZO: CHAMPIONI
prop
Wednesday, 18 April 2018
SABABU YA NYONZIMA KUTO CHEZA MECHI YATAJWA
Recommended Articles
- Michezo
Julio: Alikiba Anaweza Kucheza hata Ulaya Jun 10, 2018
KOCHA wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameweka wazi kuwa msanii wa Bongo Fleva nchini, Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’...
- Michezo
MAMBO MATANO MAKUBWA WALIO HAFIKIANA YANGA SC MKUTANO MKUUJun 10, 2018
Club ya Dar es Salaam Young Africans leo Jumapili ya June 10 2018 ilifanya mkutano mkuu na wanachama wake katika ukumbi wa Police Officers Mess M...
- Michezo
GOR MAHIA WAIPA KICHAPO SIMBA SC...SAFARI YA ULAYA NDO BASI TENAJun 10, 2018
Moja kati ya siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Bongo ni leo June 10 2018, kwani ndio ilikuwa siku inayochezwa mchezo wa...
- Michezo
MATOKEO GOR MAHIA VS SIMBA SC 2_0 KIPINDI CHAPILIJun 10, 2018
Matokeo Gor Mahia vs Simba leo 10 June 2018 Sportpesa Matokeo Gor Mahia vs Simba leo 10 June 2018 Sportpesa Matokeo Gor Mahia vs Simba leo 10 Ju...
Newer Article
Zitto kabwe ahapa kuhusu ripoti ya CAG bilioni 500
Older Article
YANGA YA SONGA MBELE KWA KUITOA DICHA MAGORI YA 2_1
Labels:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment