TUMUSIFU BWANA

prop

Monday 23 April 2018

MO SALAH AKIWA NA TUNZO YA PFA MWAKA BAADA YA USHINDI

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA).
Mchezaji huyo wa Liverpool ameshinda tuzo hiyo akimuangusha mshambuliaji wa Manchester City, Kevin De Bruyne baada ya kufunga mabao 41 katika msimu wake wa kwanza Anfield.
Leroy Sane aliyekuwa na msimu wa kipekee ndani ya Manchester City, amejinyakulia tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Grosvenor House mjini London.
Salah anakuwa mchezaji wa saba wa Liverpool kushinda tuzo hiyo na wa kwanza tangu ashinde Luis Suarez mwaka 2014.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anapewa nafasi kubwa ya kushinda Kiatu cha Dhahabu na pia anaweza kuongeza tuzo ya Mchezaji Bora wa Chama cha Waandishi wa Habari katika kabati lake, lakini kipaumbele chake ni mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya klabu yake ya zamani, Roma kesho.
"Ni heshima kubwa. Nimejituma na nina furaha kushinda hii," amesema Salah, ambaye amekuwa Mmisri wa kwanza kushinda tuzo hiyo. "Natumaini sitakuwa wa mwisho! Ninajivunia sana kushindana nimejituma sana,".
Baada ya kufunga katika sare ya 2-2 Jumamosi na West Brom, Salah amefikia rekodi ya Suarez wakilingana na Alan Shearer na Cristiano Ronaldo kufunga mabao 31 katika mechi 38 za Ligi Kuu ya England ndani ya msimu mmoja.
Na Mmisri huyo anataka aweke rekodi mpya ndani ya Liverpool katika mechi tatu zilizobaki.
"Kuvunja rekodi za Ligi Kuu England ni kitu fulani kikubwa England na duniani kote. Nataka kuvunja rekodi hii na kuvunja na nyingine (mechi 42 kwa msimu). Acha tuone nini kitatokea,"amesema Salah.

No comments:

Post a Comment