TUMUSIFU BWANA

prop

Saturday, 24 March 2018

Samia suluhu akutana na mukurugenzi wa Taasisi ya Bill & melida getes

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation, Rodger Voorhies kwenye makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi yake kwa vyombo vya habari, Makamu wa Rais amesema amezungumza mambo mengi na Voorhies hasa kwenye masuala ya afya, uwezeshaji wanawake kiuchumi, kuwatoa kwenye kilimo cha sasa na kuwaingiza kwenye kilimo biashara, lakini pia kuongeza thamani ya mazao na mambo ya masoko.

Makamu wa Rais alisema wamezungumza namna ya kuwarasimisha wanawake wa vijijini na wanawake wakulima ikiwa pamoja na uwezekano wa wanawake vijijini kuweza kupata mikopo.

Aidha, Makamu wa Rais alizungumzia suala zima la upatikanaji wa maji safi na salama, hasa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambalo mara kwa mara kumekuwa na milipuko ya magonjwa ikiwamo kipindupindu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation, Rodger Voorhies alisema wamefika kwa Makamu wa Rais kuzungumza juu ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo nchini hasa katika masuala ya kilimo na afya na Mkakati Mpya wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.

Aidha, aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua kubwa ambayo wamepiga katika kuwajumuisha wanawake katika masuala yanayohusu fedha, huku akiahidi ushirikiano mkubwa kwa Serikali ya Tanzania katika kutekelezaji wa miradi ya taasisi yao.

No comments:

Post a Comment