TUMUSIFU BWANA

prop

Saturday, 24 March 2018

Kikongwe adaiwa kubaka wanafunzi 5

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
MKAZI wa Kijiji cha Tinde katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Kachuka Malongo (90), anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi watano wa shule za msingi kwa kuwadanganya kwa pipi na fedha.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Simon Haule amethibitisha kukamatwa kwa Malongo Machi 21, mwaka huu, saa mbili na nusu asubuhi, na kueleza kuwa mtuhumiwa alikuwa akifanya kitendo hicho kwa siku na nyakati tofauti akiwadanganya kwa pipi na fedha.

Amesema, mkazi wa kijiji hicho, Amada Mgayizi (29) alibaini kubakwa kwa wanafunzi watano wa Shule ya Msingi Tinde B wakiwa wanne na mmoja Tinde A, wote walidaiwa kufanyiwa vitendo vya kubakwa na mtu mmoja kwa siku na nyakati tofauti.

Ametoa rai kwa wananchi au wazazi kuwa makini na ukaribu kwa watoto wao ili kubaini mabadiliko ya watoto na kuchukua hatua za haraka na kuonya watu wenye tabia hizo waache mara moja.

No comments:

Post a Comment