TUMUSIFU BWANA

prop

Saturday, 24 March 2018

Arusi ya mtoto wa dangote ya tikisa

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Maharusi wakiwa wamependeza.
Sherehe ya kifahari ya binti wa Bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote aitwaye Fatima Dangote, yazua gumzo nchini humo kutokana na kuhudhuriwa na watu mashuhuri kutoka sehemu mbalimbali duniani akiwemo Bilionea kutoka Marekani, Bill Gates.

Mzee Kikwete akiwa miongoni mwa waalikwa wa harusi hiyo.
Naye Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete alikuwa ni miongoni mwa wageni wa heshima waliohudhuria katika sherehe hiyo ya kihistoria.

Wengine walioudhuria ni pamoja na mke wa Rais wa sasa wa Nigeria, Hajiya Aisha Buhari; Makamu wa Rais, Osinbanjo; Spika wa Bunge, Magavana na Watu wengine mashuhuri wakiwemo wasanii na wafanyabiashara wakubwa.

Bilionea Bill Gates akiwa ndani ya ukumbi.
Davido na Wizkid waliangusha show moja kali sana mpaka mzee Dangote mwenyewe ikambidi ayarudi magoma.

Tafrija hiyo ya mapokezi baada ya ndoa (reception party) kati ya Fatima na mumewe ambaye ni mtoto wa Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu, Jamilu Abubakar, ilifanyika jana Ijumaa katika Jiji la Lagos.

No comments:

Post a Comment