TUMUSIFU BWANA

prop

Friday 8 June 2018

MCHEZAJI BORA WA MWEZI VPL ATOKEA CLABU HII APA

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.

Huyu ndiye Mchezaji bora Ligi Kuu VPL mwezi May
Mchezaji wa Azam FC ya Dar es Salaam, Shaaban Idd Chilunda, amechaguliwa kuwaMchezaji Bora wa mwezi Mei wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)Tanzania Bara.
Chilunda alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Jacob Massawe wa Ndanda na Edward Shija wa Kagera Sugar katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na kamati ya tuzo hizo.
Chilunda aliisaidia Azam akifunga mabao 6 kwa mwezi huo, ambapo kati ya mabao hayo matatu ‘hat trick’ alifunga katika mchezo mmoja.
Kwa mwezi huo Azam ilicheza michezo minne na kupata pointi tisa, baada ya kushinda michezo mitatu na kufungwa mmoja ikibaki katika nafasi yake ya pili na hakuwa na kadi yoyote.Kwa upande wa Shija aliisaidia Kagera Sugar kupata pointi 10, akifunga mabao matatu katika michezo minne iliyocheza timu yake, ikishinda mitatu na kutoka sare mmoja na kupanda kutoka nafasi ya 12 iliyokuwepo mwezi Aprili hadi ya tisa.
Massawe alitoa mchango mkubwa katika kufanikisha timu yake kuepuka kushuka daraja ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu, akiisaidia kushinda mechi mbili kati ya nne walizocheza na hivyo kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya 15hadi ya 14 katika timu 16 zilizoshiriki ligi hiyo.Kutokana na ushindi huo, Chilunda atazawadiwa tuzo, kisimbuzi cha Azam na fedha taslimu sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini Vodacom

No comments:

Post a Comment