TUMUSIFU BWANA

prop

Wednesday 4 April 2018

Miili nane ya wanajeshi wa Uganda ya rejeshwa

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Miili ya wanajeshi nane wa Uganda waliouawa katika shambulio lilitekelezwa na kundi la Al shabaab imerejeshwa nyumbani na kukabidhiwa familia zao kwa maziko.
Kwa mjibu wa msemaji wa jeshi la UPDF idadi wanajeshi wa Uganda waliouawa imeongeza hadi nane, baada ya wajeruhiwa wanne kufariki.
Jeshi la Uganda linasema zaidi ya wapiganaji 30 wa Al shabaab waliuawa katika shambulio la Jumapili.
Wanajeshi wa AU wanafanikiwa Somalia?
Gavana atuhumiwa kwa ubakaji DRC
anaelezea kuwa bendi ya jeshi la UPDF walipokea miili ya wanajeshi wa Uganda katika uwanja wa kijeshi wa Entebbe.
Naibu wa Kamanda wa majeshi ya nchi kavu Meja Jenerali Sam Kavuma ndiye aliyepokea miili ya wanajeshi wanne waliofikishwa Jumanne kuwapongeza marehemu hao kwa kazi waliofanya.
Kamanda Kavuma alisema "hawakufa bure, wamefanya kazi nzuri. Wapewe pongezi,waliweza kuwazuia wanamgambo wa Al shaabab wasifanye mashambulizi yao na kuwaangamiza."
Miili ya wanajeshi wanne walioletwa ni wale waliofariki papo hapo kwenye mapambano na kati ya majeruhi sita, wanne walifariki wakiwa hospitali na kuhitimisha idadi ya wanajeshi nane.

No comments:

Post a Comment