TUMUSIFU BWANA

prop

Wednesday 4 April 2018

Abduri nondo ahojiwa urai wake na uhamiaji

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini  (TSNP) Abdul Nondo.
Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP) Paul Kisabo amesema  kwa takribani wiki sasa Mwenyekiti  wa Mtandao huo,  Abdul Nondo,  alikuwa akihitajika Idara ya Uhamiaji ili kuhojiwa kuhusu uraia wake na wazazi wake.
Kwa mujibu wa Kisabo, Nondo ameripoti Idara ya Uhamiaji leo kwa ajili ya mahaojiano hayo.

Taarifa kamili aliyoitoa Kisabo ni hii hapa:
Kwa muda wa takribani wiki moja mpaka sasa mwenyekiti wa TSNP Abdul Nondo amekuwa akihitajika uhamiaji ili akahojiwe kuhusu taarifa za uraia wake pamoja na za ndugu zake.
Hakupata nafasi ya kwenda sababu hakuwa sawa kutokana na changamoto alizokumbana nazo.
Jana pia tulipata wito kutoka uhamiaji ili tuweze kumpeleka na akahojiwe.
Jambo hilo tumelitimiza leo tar 4.4.2018. Baada ya kutoka mahakama kuu kwenye kesi yake ambayo imeahirishwa mpaka tar 11.4.2018.
Mnamo sa sita mchana tuliweza kumfikisha Abdul Nondo makao makuu ya ofisi za uhamiaji mkoa (makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani)
Tulipata kuhoji alichoitiwa na anachotakiwa kujaza katika fomu aliyopatiwa.
Jibu tuliambiwa wanataka kupata taarifa zake binafsi, za wazazi wake, babu na bibi zake pande zote mbili (upande wa baba na upande wa mama)
pamoja na za ndugu zake,kwani Afisa uhamiaji mkoa alitamka kuwa sheria inawaruhusu kumuhoji mtu yeyote wanaotilia mashaka uraia wake .nakuwa wanamashaka na uraia wa Abdul Nondo,hivyo awathibitishie kuwa yeye ni Raia wa Tanzania.
Amejaza taarifa zile anazozifaham tu.
Baada ya hapo afisa uhamiaji aliyekabidhiwa jukum la kumhoji Abdul Nondo alisema kwamba tar 20.4.2018 Abdul Nondo anapaswa kupeleka cheti chake cha kuzaliwa, cheti cha kuzaliwa cha baba yake, mama yake, cha bibi na babu mzaa baba na mzaa mama.
Asanteni.
Paul Kisabo
Mwanasheria TSNP, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria TSNP.

No comments:

Post a Comment