TUMUSIFU BWANA

prop

Tuesday, 20 March 2018

Bunge la afrika mashariki ( EALA) Dodoma aprili 3 hadi 22

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
BUNGE la Afrika Mashariki (EALA) linatarajia kukutana mjini Dodoma kuanzia Aprili 3 hadi 22, mwaka huu. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa bunge hilo kukutana Dodoma, tangu lianze majukumu yake mwaka 2001. Likiwa Dodoma, litatumia ukumbi mmojawapo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Katika Tanzania, bunge hilo limekuwa likifanya vikao vyake katika miji ya Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar. Spika wa EALA, Martin Ngoga alilitangazia bunge lake kuwa ameshawasiliana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na ametoa kibali kwa ajili ya tukio hilo la kihistoria, ikizingatiwa katika kipindi hicho Bunge la Jamhuri ya Muungano litakuwa likiendelea na vikao vyake mjini Dodoma.

Wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo la Afrika Mashariki ni Happiness Lugiko, Adam Kimbisa, Josephine Lemoyan, Pamela Maassay, Dk Ngwaru Maghembe, Dk Abdullah Makame, Habib Mnyaa, Fancy Nkuhi na Maryam Ussi Yahya.

Majukumu ya EALA Kwa mujibu wa ibara ya 49 ya mkataba wa EAC, majukumu ya Bunge la EALA ni kushirikiana na mabunge ya nchi wanachama katika mambo yanayohusukujumuiya, kujadili na kuthibitisha bajeti ya Jumuiya.

Majukumu mengine ni kupitia na kujadili ripoti mbalimbali zinazohusu jumuiya, kujadili taarifa za hesabu zilizokaguliwa na mambo yote ya msingi ya jumuiya na kutoa mapendekezo kwa Baraza la Mawaziri kadiri itakavyoonekana inafaa kulingana na mkataba wa EAC.

Itaunda pia kamati za Bunge zikiwemo za Kamati ya Hesabu, Kamati ya Sheria, Kanuni na Madaraka ya Bunge, Kamati ya Shughuli za Kawaida za Bunge, Kamati inayoshughulikia Kanda na utatuzi wa migogoro, Kamati ya Mawasiliano, Kamati ya Biashara na Uwekezaji, Kamati ya Kilimo, Utalii na Rasilimali.

Majukumu ya kamati hizo ni kufanya kazi ya uangalizi wa utekelezaji wa mkataba ulioanzisha EAC na utekelezaji wa mkataba wa maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa katika maeneo yanayohusu ushirikiano wa jumuiya na kutekeleza majukumu mengine ya Bunge.

Bunge hilo linaundwa na wabunge 62, wakiwemo 54 wanaoziwakilisha nchi zao, tisa kila nchi. Wengine ni mawaziri wanaohusika na shughuliza EAC, Katibu Mkuu wa jumuiya na Mwanasheria Mkuu wa EAC.

Pamoja na shughuli hizo, kazi kubwa ya Bunge hilo ni kutunga sheria, kupitisha miswada mbalimbali, kufanya kazi ya usimamiziau uangalizi wa mihimili mingine ya EAC na kuwawakilisha wa eneo la jumuiya ili kusukuma mbele maendeleo ya kiuchumi kijamii, kiuchumi na mtangamano wa kisiasa.

No comments:

Post a Comment