Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
RAIS John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Blandina Nyoni kuanzia leo.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu kwa vyombo vya habari ilisema Rais Magufuli pia ameivunja Bodi ya NHC jana. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, uteuzi wa Mwenyekiti na bodi nyingine utafanyika baadaye.
Bodi hiyo imedumu madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.
Wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NHC huteuliwa na Rais, wajumbe wa bodi hiyo huteuliwa na Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Rais Magufuli alimteua Nyoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya NHC Februari 25, 2017.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(2) cha Sheria Na. 2 ya Mwaka 1990, aliwateua wajumbe 7 wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, kuanzia Machi 23, 2017.
Wajumbe walioteuliwa katika Bodi hiyo ambayo imevunjwa jana ni Profesa John Lupala, Gabriel Malata, Mary Mlay, Subira Mchumo, Ally Hussein Laay, Pius Maneno na Kesogukwele Masudi Miraji.
prop
Wednesday, 21 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment