Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amemtaka msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ asishindane na Serikali, atii sheria na mamlaka.
Waziri Mwakyembe amesikitishwa na kauli za Diamond katika kipindi cha playlist cha radio Times FM ya Dar es Salaam.
“Sheria ni ya watu wote bila kujali umaarufu au nafasi ya mtu katika jamii, hivyo msanii Diamond anapaswa kutii sheria na mamlaka zilizowekwa” imesema taarifa ya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katika kipindi hicho Diamond alishutumu hatua ilizochukua Serikali kutunza na kulinda maadili ya Kitanzania kwenye tasnia ya sanaa na muziki.
Kwa mujibu wa Waziri Mwakyembe, uamuzi wa kuzifungia nyimbo na wasanii wawili kwa kukiuka maadili ulifanywa kwa kuzingatia sheria na haukuwa utashi wa Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juliana Shonza.
Dk. Mwakyembe amesema, Diamond anapaswa kutambua kuwa, Serikali ina taratibu zake na uamuzi wa Naibu Waziri ni wa Wizara na kama ana ushauri awasilishe kwa utaratibu sahihi na si kwa kumshambulia msaidizi wake kwa dharau na kejeli.
prop
Wednesday, 21 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment