TUMUSIFU BWANA

prop

Wednesday, 21 March 2018

Abdul nondo apandishwa kinzimbani leo

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo amepandishwa mahakamani leo katika mahakama ya wilaya ya Iringa mjini ambapo anashatakiwa kwa kosa la kudanganya kuwa alitekwa na kudaiwa kutoa taarifa za uongo mtandaoni.
Leo ni siku ya 21 tangu kushikiliwa kwa mwanafunzi huyo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baada ya kufikishwa mahakamani kijana huyo amenyimwa dhamana na hakimu mkazi wa mahakama hiyo kwa sababu ya "usalama wake kuwa hatarini".
Imeelezwa kuwa kupewa dhamana kunaweza kuleta hatari zaidi, aidha hakimu huyo ameahirisha kesi hadi siku ya Jumatatu ili aweze kupitia vifungu vya sheria na kujihakikishia kama ni salama kumuachia kwa dhamana au la
Wakati mwanafunzi huyo akiwa mahakamani mkoani Iringa kesi nyingine iliyofunguliwa na jopo la mawakili wake wakiongozwa na wakili Mpale Mpoki juu ya utaratibu mzima wa kukamatwa kwa kijana huyo pamoja na suala la dhamana, ilikua inaendelea katika mahakama kuu jijini Dar es salaam na kuahirishwa hadi tarehe nne mwezi wa nne ili pande zote ziwasilishe nyaraka zao.
Kesi hiyo ilifunguliwa dhidi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI), Mwanasheria mkuu wa serikali na mkuu wa jeshi la polisi IGP kwa madai ya kuchelewesha kumshtaki mahakamani mwanafunzi Abdul Nondo na kumnyima dhamana bila sababu ya msingi.

No comments:

Post a Comment