Moja kati ya siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Bongo ni leo June 10 2018, kwani ndio ilikuwa siku inayochezwa mchezo wa fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 kwa kuzikutanisha timu za Simba SC dhidi ya Gor Mahia.
Game ya fainali ilichezwa katika uwanja wa Afraha Nakuru nchini Kenya lakini kikubwa ukiachilia mbali zawadi ya Kombe na pesa, zawadi ya Bingwa kwenda katika jiji la Liverpool England katika uwanja wa Goodson Park iliongeza hamasa na mvuto wa game yenyewe.
Bahati mbaya Simba ambao ndio walikuwa wawakilishi pekee wa Tanzania katika mchezo huo wa fainali, wamejikuta wakipoteza nafasi ya kucheza na Everton baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-0, hivyo Gor Mahia wanatetea Ubingwa wao na watacheza tena kwa mara ya pili game ya kirafiki na Everton.
Kingine kilichokuwa kinaleta mvuto ni kuwa Simba SC ilikuwa inacheza na Gor Mahia ambayo inafundishwa na kocha Dylan Kerr raia wa England, kocha ambaye aliwahi kuifundisha Simba miaka ya nyuma ila walimfuta kazi baadae kwa kutoridhishwa na mwenendo wa timu.
No comments:
Post a Comment