TUMUSIFU BWANA

prop

Monday, 9 April 2018

Matokeo ya mechi ya mtibwa vs simba 0_1

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.


Wachezaji wa Timu zote wanaingia uwanjani wakiongozwa na waamuzi wa Mchezo wa Leo

Wachezaji wanasalimiana na Mgeni rasmi wa Mchezo wa LEO

Nyavu za uwanja wa Jamhuri ndizo zinakuwa Kikwazo kwa mchezo kuanza mwamuzi msaidizi yupo anaziweka sawa, zinaonekana kutokuwa sawa kutokana na baadhi ya maeneo kuwa na Matundu mapana

Mechi imeanza katika uwanja wa Jamhuri Morogoro,  baada ya Nyavu kufungwa na bandage , Mtibwa 0 – 0 Simba

Dakika ya Kwanza Stahimil Mbonde alikuwa anaambaaambaa na Mpira lakini akakutana na Kisiki cha Yusuph Mlipili

Golikipa Tinocco alitaka kufanya masihara mbele ya Bocco anaokolewa na Miguu yake mara baada ya Kuutema Mpira mbele ya Bocco, Yupo chini kaumia anatibiwa

Dakika ya 4 Shomari Kapombe anapiga shuti linakwenda Nje ya Lango, Bado ni 0 kwa

Dakika ya 8 Timu zote zinaonekana kucheza kwa Kusomana matokeo yakiwa 0 kwa 0

Dakika ya 9 Mvua Imeanza Kunyesha uwanjani  lakini bado mechi inaendelea kuchezeka, 0 kwa 0

Dakika ya 11 Kichuya akiondoka na Mpira anawekwa chini, Refa anaona ilikuwa nyepesi anapeta

Dakika ya 14 Mtibwa wanapata Kona ya kwanza na kona ya kwanza kwenye mchezo, 0 kwa 0

Dakika ya 15 Shiza Kichuya anawachukua mabeki wa Mtibwa anapiga Krosi inakutana na Okwi  inambabatiza na Kutoka nje

Dakika ya 19 Henry Joseph yupo chini baada ya kujigonga goti kwenye mwili wa Shomari Kapombe, Mtibwa 0 – 0 Simba

Henry Joseph anarejea uwanjani

Dakika ya 23 Emmanuel Okwi anaipatia Simba bao la Kuongoza katika uwanja wa Jamhuri, Ilipigwa Majalo na Shiza Kichuya, John Bocco akapiga kwa Kichwa na Mpira ukamkuta Okwi aliyekuwa Peke Yake na Okwi kaweka Kambani kwa Mguu akiwa Free

Mtibwa 0 – 1 Simba

Dakika ya 28 Hassan Dilunga anakokota mpira na Kupiga Shuti linaloenda nje ya Lango

Dakika ya 29 Mtibwa wanapata Mpira wa Adhabu

Dakika ya 30 Mpira wa adhabu unapiwa unatolewa na Kuwa Kona, Kona inakosa madhara kwa Simba

Dakika ya 32 Hassan Dilunga na Jonas Mkude wanaonyeshwa kadi za Njano mara baada ya kuvimbiana  na Kuonyeshana ubabe

Dakika 35

Mtibwa 0 – 1 Simba (Dakika 23 Emmanuel Okwi)

Dakika ya 37 Kihimbwa anajaribu shuti la Nje ya 18 Manula anaokoa Inakuwa Kona, Kona Inapigwa Simba wanakoswa Goli hapa.

Ilipigwa kona Henry Joseph akapiga Kichwa ukataka Kuingia ukaokolewa Kikapigwa Kichwa Tena mpira Ukagonga mwamba wa Juu ukarudi.

Dakika ya 39 Ikapigwa tena kona mchezaji wa Simba akaonekana kuushika lakini refa akapeta, Bado Mtibwa 0 – 1 Simba

No comments:

Post a Comment