TUMUSIFU BWANA

prop

Thursday, 22 March 2018

Kikosi cha Ethiopia kitakacho cheza na yanga shirikisho

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Wolaitta Dicha F.C ni timu iliyoanzishwa mwaka 2009 na imepanda kucheza Ligi Kuu Ethiopia kwa mara ya kwanza msimu wa 2013/2014 hivyo huu ni mwaka wake wa nne kucheza Ligi Kuu Ethiopia ambapo haijawahi kutwaa taji hilo zaidi ya Ethiopian Cup iliyotwaa kwa mara ya kwanza mwaka jana.

Club ya Wolaitta Dicha F.C imefuzu kucheza hatua hiyo kwa kuiondoa club Kongwe na yenye historia kubwa katika soka la Afrika Zamalek ya Misri kwa mikwaju ya penati 3-4, hiyo ni baada ya kucheza game zote mbili nyumbani na ugenini na kumalizika kwa kila mmoja kupata ushindi wa 2-1 akiwa nyumbani, wakati round ya kwanza ilipita kwa kuitoa Zimamoto ya Zanzibar, hivyo Yanga  anapewa nafasi kwa kuwa na uzoefu wa game za kimataifa.

No comments:

Post a Comment