Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima ameanza mazoezi na wenzake baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha. Niyonzima alikwenda india kwa ajili ya matibabu ambapo ilielezwa angefanyiwa upasuaji mdogo lakini jambo zuri ni kwamba alitibiwa bila kufanyiwa upasuaji.
Niyonzima anaamini baada ya muda mfupi atarudi uwanjani baada ya kumaliza program za mwalimu.
“Siwezi kuja mazoezini kabla sijawa vizuri, lakini siwezi kuesema nipo vizuri kwa 100% watau wanachotakiwa kujua, mtu ukitoka kwenye maumivu huwezi kuja kujiunga na timu moja kwa moja lakini ninachoshukuru naona kama napiga hatua kwa sababu siku za nyuma nilikuwa nyumbani lakini sasa nimeanza kuungana na timu.”
“Kwa sasa najisikia nafuu na nimeanza kupewa ratiba na mwalimu naamini mambo yatakuwa mazuri. Kuna ‘recover’ za ina mbili kuna ya daktari na mwalimu, ya daktari tayari nimeshafanya sasa hivi nafanya ya mwalimu kwa hiyo ikiisha najiunga na timu.”
“Nimemi-miss kucheza kwa sababu muda mrefu sijacheza na watu wanajua mpira ni kazi yangu lakini siwezi kuchukua uamuzi nikasema nacheza, natakiwa kwenda na ratiba ya timu, daktari na mwalimu lakini sasa hivi nipo kwenye ratiba ya mwalimu, muda si mrefu nitarudi uwanjani.”
prop
Monday, 26 March 2018
Nyonzima kulejea simba Leo
Recommended Articles
- Michezo
Julio: Alikiba Anaweza Kucheza hata Ulaya Jun 10, 2018
KOCHA wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameweka wazi kuwa msanii wa Bongo Fleva nchini, Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’...
- Michezo
MAMBO MATANO MAKUBWA WALIO HAFIKIANA YANGA SC MKUTANO MKUUJun 10, 2018
Club ya Dar es Salaam Young Africans leo Jumapili ya June 10 2018 ilifanya mkutano mkuu na wanachama wake katika ukumbi wa Police Officers Mess M...
- Michezo
GOR MAHIA WAIPA KICHAPO SIMBA SC...SAFARI YA ULAYA NDO BASI TENAJun 10, 2018
Moja kati ya siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Bongo ni leo June 10 2018, kwani ndio ilikuwa siku inayochezwa mchezo wa...
- Michezo
MATOKEO GOR MAHIA VS SIMBA SC 2_0 KIPINDI CHAPILIJun 10, 2018
Matokeo Gor Mahia vs Simba leo 10 June 2018 Sportpesa Matokeo Gor Mahia vs Simba leo 10 June 2018 Sportpesa Matokeo Gor Mahia vs Simba leo 10 Ju...
Labels:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment