TUMUSIFU BWANA

prop

Monday 26 March 2018

Luuondo amfungia safari bushoke

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
STAA wa Muziki wa Harakati, Luundo Dunia amemfungia safari upya mkali wa Bongo Fleva, Bushoke kwa ajili ya kufanya naye kazi nyingine ya muziki.

Akizungumza leo mchana mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Luundo alisema moja ya sababu za kuwasili nchini ni kufanya tena kolabo na Bushoke pamoja na msanii mwingine.

Alisema kuwa, wimbo aliofanya na Bushoke uitwao Mbegu za Amani umetokea kukubalika zaidi nchini Canada hivyo akaona ni vyema kutengeneza naye kazi zingine.

“Bushoke anapendwa sana Canada na wimbo wetu wa Mbegu za Amani umependwa sana, lakini mbali na kuja kufanya naye kazi pia nitafanya kazi na msanii mkubwa wa Injili Tanzania anaitwa Christina Shusho,” alisema Luundo.

No comments:

Post a Comment