Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Katibu Mkuu wa Chama Cha wanachi (CUF), Maalif Seif Sharif Hamad, akizungumza na wanachama wa chama hicho (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Mkutano na wanachama ukiendelea.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha wanachi (CUF) , Maalif Seif Sharif Hamad amemtolea uvivi Mwenyekiti wa Chama hicho anayeungwa mkono na Msajili wa Vyama vya siaa, Prof. Ibrahimu Lipumba akimtaka kuacha kukivuruga chama hicho kwani muda walionao kwa sasa ni kukijenga chama hicho.
Maalim ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wake na wanachama wa chama hicho uliofanyika katika Hoteli ya Korini iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wanachama wake kuwa wamoja na kutoyumbishwa na upande wa Lipumba.
Amesema kuwa Lipumba ni mtu asiyekuwa mkweli, kwani yeye ndiye aliyempokea Edward Lowassa katika UKAWA lakini siku chache baadae akageuka na kudai kuwa hakubaliani na maamuzi ya kumkaribisha katika umoja huo.
Mkutano baina ya Katibu mkuu wa chama hicho na wanachama hao ulikuwa na lengo la kujenga mshikamano na umoja ndani ya chama hicho.
prop
Saturday, 24 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment