TUMUSIFU BWANA

prop

Saturday, 24 March 2018

Ronaldo alicho mfanyia mo salah atokisahau

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
MWANASOKA bora wa dunia anayeichezea Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kuonesha ubabe wake mbele ya nyota wa Misri, anayefanya vizuri kwasasa na klabu yake ya Liverpool, Mohamed Salah baada ya kuisawadhishia Ureno na kufunga bao la ushindi katika mechi baina ya timu hizo za taifa.

Ronaldo ameonesha umwamba huo kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA ambapo timu yake ya Ureno ilikuwa mwenyeji wa Misri na ilikubali kuwa nyuma kwa bao la Salah hadi dakika ya 90 kabla ya Ronaldo kubadili mambo.

Salah aliitanguliza Misri kwa bao la dakika ya 56 kisha Ronaldo kuamua ushindi wa mabao 2-1 kwa timu yake ya Ureno kwa mabao ya dakika ya 90+2 na 90+4.

Baada ya mabao hayo mawili Ronaldo sasa amefikisha jumla ya mabao 81 ya kuifungia timu yake ya taifa akiwa ndio mchezaji mwenye mabao mengi zaidi akifuatiwa na Messi mwenye mabao 61 aliyoifungia Argentina.

Mohamed Salah kwasasa ndio anaongoza mbio za ufungaji bora kwenye ligi kuu soka ya England akiwa na mabao 28, wakati Ronaldo ana mabao 22 kwenye ligi kuu ya soka Hispania.

PORTUGAL (4-4-2): Beto, Cedric, Rolando, Bruno Alves, Guerreiro, Neves, Bernardo Silva (Gelson Martins 68), Joao Mario (Quaresma 61), Joao Moutinho (Andre Gomes 61), Ronaldo, Andre Silva (Goncalo Guedes 76)


Subs not used: Rui Patricio, Neto, Fonte, Fernandes, Rui, Adrien Silva, Cancelo, Bruno Fernandes, Lopes
Goals: Ronaldo 90+2, 90+5

Booked: Alves
EGYPT (4-3-3): El Shenawy, Fathi, Gabr, Hegazi, Abdel-Shafy, Hamed (Ashour 87), Elneny, Said (Warda 66), Trezeget, Salah (Shikabala 79), Hassan (Mohsen 62)
Subs not used: Al Shenawy, Elmohamady, Morsy, Kahraba, Zakaria, Sobhi, Samir, Ashraf
Goals: Salah 56
Booked: Fathy
Referee: Paolo Mazzo

No comments:

Post a Comment