TUMUSIFU BWANA

prop

Friday, 23 March 2018

China na India kuwekeza ujenzi wa viwanda vya nakshi dodoma

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
WAWEKEZAJI kutoka China na India wanatarajia kujenga viwanda viwili katika vijiji vya Itiso na Ntyuka mjini Dodoma ambavyo vitazalisha na kuuza ndani na nje nakshi zinatokana na mawe.

Viwanda hivyo vitakavyogharimu mamilioni ya dola za Marekani, vinatarajiwa kuwa vimekamilika mwakani.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko amewaeleza waandishi wa habari baada ya kufanya ziara katika migodi ya uchimbaji mawe ya nakshi katika eneo la Ntyuka katika Manispaa ya Dodoma na yale ya Itiso wilayani Chamwino.

Wakati uzalishaji wa Ntyuka umelenga hasa soko la ndani hususani kwa matumizi ya jikoni na sakafuni, wawekezaji wa Itiso wameamua kujenga kiwanda nchini baada ya kusitishwa kwa usafirishaji wa mawe yasiyoongezewa thamani kwenda nje tangu mwaka 2017.

Uamuzi wa kusitisha usafirishaji mawe hayo ulitokana na agizo la Rais John Magufuli ambaye alipiga marufuku usafirishaji wa makinikia nje ya nchi na kutaka kuwepo uongezaji wa thamani ambao utafanyika nchini.

“Tulizuia usafirishaji wa madini ghafi kama sheria ya nchi ilivyotaka. Tulitaka wawekezaji wote kuongeza thamani kabla ya kusafirisha, hatua hii itaongeza ajira na kuinua uchumi wa nchi,” amesema Biteko.

Kwa mujibu wa Mtanzania ambaye ni mbia katika mgodi wa Itiso, Sisti Mganga, Watanzania ni asilimia 10 na Wachina asilimia 90, na kwamba kuna malighafi za kutosheleza kiwanda wanachotaka kujenga na itakuwa kituo kwa ukanda wa kati.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Udbhav International Ltd ambayo inamiliki asilimia 70 ya mgodi wa Ntyuka, Sweekar Nayak alisema wako tayari kuanza ujenzi wa kiwanda muda wowote kuanzia sasa.

Amesema, kwa sasa wameanza kupata soko la ndani kwa kuwauzia kampuni inayojenga Jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini hapa ambapo huuza kati ya vipande 300 hadi 400 kwa mwezi vya nakshi za mawe. Naye Ofisa Madini Mkazi wa Dodoma, Silimu Mtingile alisema wawekezaji hao wamepewa leseni za kuendesha shughuli hizo na kuwa sasa mamlaka za serikali zinafanyia kazi taratibu za kisheria ili wafungue viwanda.pakua app Yetu kalambonews uhabarike Kwa kilatukio linalotokea kila siku

No comments:

Post a Comment