Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa kimetumia zaidi ya Sh milioni 18 ndani ya wiki tatu kutekeleza ahadi iliyotolewa miaka miwili iliyopita na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kwa wanajumuiya wa Soko Kuu la mjini Iringa.
Katika moja ya mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Mchungaji Msigwa aliiahidi jumuiya hiyo kununua Televisheni seti za kisasa 10 zitakazofungwa katika soko hilo ili ziwawezeshe pamoja na wateja wao kufuatilia mambo mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya nchini.
Februari 28, mwaka huu CCM ilianza kufuta machozi ya wanajumuiya hiyo kwa kupeleka televisheni moja aina ya Sumsung ya inchi 58 pamoja na king’amuzi cha Azam kabla ya kuombwa iongeze nyingine kwa kuzingatia ukubwa wa soko hilo.
Katika kujibu mapigo ya CCM, wiki moja baadaye, Machi 10 mwaka huu, Mchungaji Msigwa alifanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa na kuwahahakishia wapiga kura wake kwamba ahadi aliyoitoa kwa wafanyabishara wa soko hilo ipo pale pale.
Wiki moja baada ya ahadi ya Mchungaji Msigwa, CCM walipeleka televisheni nyingine tano aina ya Samsung, nne zikiwa za inchi 43 na moja ya inchi 65, ving’amuzi vyake na Sabu wufa ambazo matumizi yake katika pembe tofauti za soko hilo yalizinduliwa jana na Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Iringa, Said Rubeya.
Akizindua matumizi ya televisheni hizo huku akishangiliwa na baadhi ya wafanyabiashara na wateja wa soko hilo, Rubeya alisema; “Tunampa mwezi mmoja Mchungaji Msigwa kuwaletea Televisheni nne zilizobaki katika ahadi yake ya kuleta televisheni 10, akishindwa tutamalizia wenyewe.”
Rubeya alisema CCM siyo chama cha blabla, kinawathamini Watanzania na kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, kinafanya kila kinaloweza kushughulikia changamoto mbalimbali za wananachi.
Awali Katibu wa CCM wa Manispaa hiyo, Marko Mbanga alisema CCM imetekeleza ahadi hiyo baada ya kupokea kilio kutoka kwa jumuiya hiyo kwamba Mbunge Msigwa amekuwa akiwapiga danadana kuitekeleza pamoja na kurudia kuahidi mara kwa mara. "Kalambonews for you now''. Install now
prop
Friday, 23 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment