TUMUSIFU BWANA

prop

Wednesday 28 March 2018

Chadema watoa tamko leo

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
IKIWA ni saa 24 tangu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake  wafikishwe mahakamani na kuswekwa rumande baada ya kunyimwa dhamana, Kamati Kuu ya chama hicho imetoa msimamo wake leo na kudai kuwa hawapo tayari kuendelea  kuonewa.

Baadhi ya viongozi wa Chadema waliozungumza ni pamoja na Makamu mwenyekiti wa Chadema, Profesa Safari, Godbless Lema na John Mrema, ambapo mkutano huo pia umehudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Kuu akiwemo Edward Lowassa, Fredrick Sumaye na Meya Boniface Jacob.

Akizungumza leo Machi 28 na wanahabari jijini Dar, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Abdallah Safari amesema tukio la kunyimwa dhamana na kupelekwa rumande kwa viongozi hao ni uonevu kwani dhamana ni haki ya mtuhumiwa anapokamatwa.

“Licha yaa jitihada za mawakili wetu kuwatetea viongozi wetu lakini wamewanyima dhamana. Tumemwandikia barua Jaji Mkuu kumwambia mbona kila tunapokamatwa linapofika swala la dhamana tunakataliwa? Jaji Mkuu kajibu kirahisi sana eti kateni rufaa,” alisema Prof. Abdallah Safari.

Aidha, ameagiza madiwani wote wa chama hicho nchini kushirikiana na wanachama wote wa Chadema kufanya vikao na kutoa tathmini ya hali inavyoendelea sambaba na kutoa mwelekeo wa nini kifanyike ili kukomesha mambo hayo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema:
“Huo mchezo wanaotaka kufanya waendelee nao, wamewanyima dhamana ili kesi iendeshwe haraka na wawafunge kama alivyofanyiwa Sugu. Tunajua vikao vyao na nia yao. Wakitaka tusema, ukiogopa kufa utakufa.

“Sisi tutaweka mambo mengi hadharani, sina uhakika kama Mwenyekiti wetu kesho atapewa dhamana. Hapa tulipofika hatuwezi kuendelea kuishi kwa hofu. Hii vita si ya Chadema, hii ni vita ya demokrasia, Akwilina hakuwa mwanachama wa Chadema lakini aliawa, sasa nafikiri inatosha.

“Baada ya kutoka mahakamani kesho tutakutana na kuamua iwapo tufungulie maji na tuanike kila kitu kwa sababu hatuna namna. Yeyote aliyehusika tutamuanika,” alisema  Lema.

No comments:

Post a Comment