TUMUSIFU BWANA

prop

Friday, 8 June 2018

TFF YAIPA YANGA SIKU MBILI KUTENGUA UAMZI WAO KUJITOA KAGAME CUP

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
TFF yaigomea Yanga kujitoa Kagame yatoa saa 48 kwa Yanga


TFF yaigomea Yanga kujitoa Kagame yatoa saa 48 kwa Yanga
Soma hapa kurasa za magazeti ya Leo jumamosi
Rais wa TFF Wallace Karia ameujia juu Uongozi wa Yanga na Kushangaa sababu wanazotoa za kutoshiriki michuano ya Kagame

Karia ameutaka Uongozi wa Yanga kukaa chini na ndani ya saa 48 Kukaa na Kutengua Kauli ya Kujiondoa kwenye mashindano hayo kwani sababu walizotoa hazina mashiko.

Tamko la Gor Mahia baada ya Kusikia Yanga inataka wachezaji wao
“Sababu walizozitoa Yanga juu ya kutoshiriki michuano ya Kagame hazina mashiko, maana si Yanga peke yao ambao ratiba imewabana na ukiangalia hiyo michuano ya Shirikisho Afrika hata Gor Mahia pia wapo, mashindano ya Sportspesa Super Cup ambayo mpaka hivi sasa Gor Mahia wapo na wanacheza fainali Jumapili na Simba,”

alisema Rais Wallace Karia na kuongezea; “Hivyo kabla hata hatujalipeleka suala hili CECAFA, nauomba uongozi wa Yanga hadi kufika jumapili uwe umetoa jibu la kueleweka juu ya mashindano hayo,”

No comments:

Post a Comment