TUMUSIFU BWANA

prop

Friday, 8 June 2018

HIVI APA VYUO 20 VILIVYOFUNGIWA NA NECTA NA SABABU ZA KUFUNGIWA

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
 Vifahamu vyuo 20 vilivyofungiwa na NACTE na sababu za kufungiwa


Leo June 8, 2018 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limefuta usajili wa vyuo 20 kwa kushindwa kufuata utaratibu wa usajili wa vyuo vya ufundi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kufuata utaratibu wa usajili wa vyuo vya ufundi na upungufu wa rasilimali za kufundishia

Pia Baraza limezuia vyuo 9 kudahili wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo 2018/19 na vyuo 3 vimesitishwa kutoa program zisizohidhinishwa na Baraza hilo.



Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dr. Adolf Rutayuga amesema vyuo hivyo bado vina nafasi ya kuomba usajili upya endapo watarekebisha matatizo na utaratibu ukafuatwa.

“Matokeo ya uchunguzi uliofanywa kuanzia July 2017 mpaka September 2017 ambao ulihusisha vyuo 458 ambapo 112 vya ualimu na vingine 7 vilivyokutwa haviendelei na shughuli za elimu, vyuo 426 vimekidhi vigezo lakini vyuo 32 vimekutwa na mapungufu hivyo Baraza limechukua hatua mbalimbali kwa vyuo hivyo 32,”  Dr Rutayunga

Toa maoni yako niya mhimu pia unaweza kumshirikisha mwenzio au jama yako sasa .

No comments:

Post a Comment