TUMUSIFU BWANA

prop

Wednesday, 23 May 2018

Meneja wa Diamond arudishwa rumande tena

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa mwanamuziki Naseeb Abadul ‘Diamond’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ (katikati aliyekaa) akiwa na wakili wake na ndugu zake mahakamani hapo.
Mahakama hiyo pia leo ilitoa fursa kwa pande mbili zinazohusika katika kesi hiyo kujadiliana lakini baada ya majadiliano hayo pande zote zilirudisha majibu kwa hakimu kwamba hazikufikia maelewano yoyote.  Hivyo msajiri wa Mahakama Kuu alichukua uamuzi wa kuiahirisha tena kesi hiyo.
Soma magazeti ya Leo alhamisi bofya hapa
…Wakiendelea kuongea.
Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

No comments:

Post a Comment