TUMUSIFU BWANA

prop

Monday 23 April 2018

Tetesi za usajili Tanzania jumatatu ya 23.2018

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Usajili : Ishu ya Yanga kumsajili Adam Salamba wa Lipuli

Yanga ni kama inataka kujiimarisha zaidi hasa kwenye safu yake ya Ushambuliaji ambayo kwa msimu huu imekuwa siyo Kisu Kikali kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita.

>>Habari za Michezo bonyeza hapa <<

Kuna Tetesi kuwa Tayari Kamati ya Usajili klabu ya Yanga imeanza Mazungumzo na mchezaji Adam Salamba wa Lipuli ili kuweza kumsajili kwaajili ya Msimu ujao wa Ligi na mashindano ya Kimataifa.

Taarifa zaidi zinasema klabu ya Yanga imeona iwahi mapema kumalizana na mchezaji huyo ili kuwawahi WAPINZANI wao Simba ambao wanaweza kumuwahi kutokana na Kuonekana kuwa straika mzuri mwenye nguvu, akili na uwezo mkubwa wa Kufunga.

Salamba  msomaji wa Kwataunit ndiye aliyekuwa Mwimba Mchungu kwa Simba mara baada ya Kuwafunga bao akimgeuza anavyotaka Beki Yusuph Mlipili na Kupachika bao Lipuli ikicheza na Simba.

Kama mambo yataenda vizuri huenda Yanga wakavunja Kibubu ili kuhakikisha Salamba ananza kucheza kwenye michuano ya Kimataifa hatua Ya Makundi kombe la Shirikisho ambapo itabidi wavunje mkataba wa Salamba na Lipuli.

Adam Salamba alijiunga na Lipuli wakati wa Dirisha Dogo akitokea katika klabu ya Stand United Chama la Wana kutoka mkoa Shinyanga.

Na Toka atue Lipuli amekuwa mchezaji muhimu na hatari kwenye safu ya Ushambuliaji, ikumbukwe huyu Pia ndiye Mchezaji bora wa Mwezi March wa Ligi kuu soka ya Tanzania bara Vodacom Premier League.

No comments:

Post a Comment