TUMUSIFU BWANA

prop

Tuesday 24 April 2018

TETESI ZA USAJILI BALANI ULAYA JUMANNE YA 24.2018

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Manchester City wako tayari kumuachia mlinzi wa England John Stones, mwenye umri wa miaka 23, msimu huu wa joto. (Sun)
Mshambuliaji wa Tottenham Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 33, ana nafasi ya kuondoka katika klabu hiyo na huedna akajiunga tena na klabu yake ya zamani Athletic Bilbao. (Mirror)
Manchester City wanaongoza jitihada za kumsajili mchezaji wa Napoli raia wa Italia mwenye umri wa miaka 26 Jorginho na mabingwa hao wa Premier League wamefanya mazungumzo ya kina na wawakilishi wa mchezaji huyo. (Mail)

Alex Iwobi ni mojawapo ya wachezaji wa Afrika waliofunzwa na Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal
Mrithi wa Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal itabidi atumei bajeti ndogo msimu huu wa joto ya kiasi ya £ milioni 50. (Telegraph)
Mkurugenzi mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis anaamini kuwa kapteni wa zamani wa Gunners Mikel Arteta, mwenye umri wa miaka 36, ambaye sasa ni kocha katika timu ya Manchester City, huenda akawa ndiye mrithi wa Arsene Wenger. (Sky Sports)

No comments:

Post a Comment