TUMUSIFU BWANA

prop

Monday 30 April 2018

MATOKEO YA MWADUI FC VS MBAO FC VPL 1_0

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Matokeo Mwadui Fc vs Mbao Fc VPL 30 April 2018

Matokeo Mwadui Fc ambao wapo nyumbani kuwakaribisha Timu ya Mbao Fc kutoka Jijini Mwanza, timu zote zinapambana ili kutoshuka Daraja

Mwamuzi Erick Onoka anapuliza Filimbi kuahiria kuanza kwa pambano.

Dakika ya Kwanza Mbao wanapata Kona, kona inapigwa refa anasema Irudiwe.

Inapigwa Kona lakini Inashindwa kuleta madhara langoni mwa Mwadui Fc.

Dakika 5 Zimekatika

Mwadui Fc 0 – 0 Mbao Fc

Dakika ya 7 Mbao wanapata kona ya Pili kwenye mchezo Huu, Lakini mabeki wa Mwadui wanaokoa lakini Mpira bado upo Langoni mwa Mwadui

Dakika ya 8 Mwadui wanafanya shambulizi zuri kipa anatoa na Kuwa Kona

Mwadui 0 – 0 Mbao Fc

Dakika 15

Mbao wanaonekana kucheza vizuri wakiwa wamerelax wakipiga pasi Fupi na Kutengeneza mashambulizi kadhaa, Lakini bado ni 0 kwa 0

Dakika ya 17 Mwadui wanapata kona, Mabeki wa Mbao wanaokoa Mpira Unarudi tena Langoni mwa Mbao ni hatari lakini Unaokolewa tena

Dakika ya 26 Mwadui wanafanya Shambuzi la Kiume, Unapigwa Mpira Unagonga Mwamba wa Juu unatoka

Mwadui 0 – 0 Mbao Fc

Dakika ya 29 Makosa ya safu ya Ulinzi ya Mbao yanawapa Mwadui bao la Kuongoza.

Mwadui 1 – 0 Mbao Fc

Awesu anapewa kadi ya Njano baada ya Kumwadaa mwamuzi kuwa amekanyagwa kumbe kajiangusha

Dakika 35

Mwadui 1 – 0 Mbao Fc

Dakika ya 42 Gerald Mathias wa Mwadui anapewa kadi ya Njano, Alionekana anachonga sana kwa Mwamuzi

Mpira ni mapumziko

Mwadui 1 – 0 Mbao Fc

KIPINDI CHA PILI

Dakika ya 46 Kipa wa Mbao anapewa kadi ya Njano kwa kucheza Faulo

Dakika ya 49 Salum Hamis wa MWADUI anakosa bao yeye na Kipa wa Mbao Hassan Mohammed, Kipa anaokoa

Dakika ya 52 Kipa wa Mwadui Emmanuel Massawe anapewa kadi Nyekundu baada ya KWENDA kuukoa Mpira Uliokuwa unaelekea Golini nje ya 18

Dakika ya 56 Mwadui wanafanya Sub ili aweze Kuingia kipa mwingine

Dakika ya 70

Mwadui 1 – 0 Mbao Fc

Dakika ya 75 Mbao wanapata Kona mwadui wanaokoa

No comments:

Post a Comment