Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Mchezaji Yanga apata timu Ubelgiji
KLABU ya Bevelen ya Ubelgiji imeanza mchakato wa kumsajili winga machachari wa Yanga, Emmanuel Martin kwenye kikosi chake baada ya kuvutiwa na soka lake.
Bevelen inamtaka Martin kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya nchi hiyo ambayo straika na nyota wa Tanzania, Mbwana Samatta ndiko anakokipiga. Pia, timu hiyo ilimsainisha mdogo wa kiungo wa Simba Haruna Niyonzima, Bizimana Djihad aliyekuwa APR.
Klabu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza imeshatuma watu wake kwa ajili ya kumfuatilia mchezaji huyo huku ikiendelea kumfuatilia katika mechi zake Ligi Kuu na zile za Kombe la Shirikisho Afrika ambayo Yanga inashiriki katika hatua ya makundi.
“Ni kweli Bevelen inamhitaji Emmanuel Martin na imeshaanza kumfuatilia katika michezo yake mbalimbali pamoja na mazungumzo ya awali, mipango zaidi inategemea kuifanya baada ya mechi yao na Rayon,” alisema mtu wa karibu na klabu hiyo.
Chanzo hicho kilifichua kuwa, makubaliano yao ni kwamba, Martin ataenda kufanya majaribio na baada ya hapo, ndiyo mambo mengine ya kimkataba yataendelea.
Alipotafutwa Martin alikiri kupewa mchongo huo wa kijanja kwa kusema; “Unajua mambo haya hayajawa rasmi, usiwe na haraka dada ndiyo maana nashindwa kuyatolea maelezo kwa sasa, kama yatakuwa tayari nitaweza kuyazungumzia kwa undani zaidi.”
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema:
“Sisi tunachohitaji kwa timu yeyote inayomuhitaji ije na ifuate utaratibu. Taratibu zinajulikana inaandikwa barua na wanamtaja mchezaji wanayemuhitaji, kama ni majaribio kwa muda gani na sisi tunalifanyia kazi suala lao na kuwajibu.”
“Lakini si kupitia mlango wa nyuma kama wanataka kumuiba, hatutaweza kukubali,”
alieleza Mkwasa na kufafanua ameisiakia suala la Martin juujuu likizungumzwa kama mwandishi alivyouliza lakini jamaa hao hawajafika mezani.
source : Mwanaspoti
prop
Friday, 11 May 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment