TUMUSIFU BWANA

prop

Saturday 5 May 2018

Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya USM Alger Leo 6 May 2018

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya USM Alger 6 May 2018

Kulingana na Kikosi cha Yanga ambacho Kipo nchini Algeria tayari kwa Mchezo dhidi ya USM Alger hki ndicho Kikosi cha Yanga Kinachoweza Kuanza dhidi ya USM Alger katika Mchezo wa leo.

Kipa : Nafasi ya Kipa bila Shaka Youthe Rostand Jehu ambaye amekuwa kipa katika kikosi cha Yanga msimu Huu Ataendelea kuaminiwa na benchi la Ufundi huku Ramadhan Kabwili akiwa kama Mbadala wake Nje.

Mabeki wa Pembeni : Kulia naona nafasi ya Juma Abdul na siyo Hassan Kessy kwanini Juma Abdul, Kwenye mechi kama hii ya Ugenini Abdul anaweza kuwa Mzuri zaidi kwani hauhitaji mchezaji mwenye makosa mengi yanayoweza sababisha kadi,

Lakini Pia unahitaji kutengeneza nafasi chache zenye faida kwa mfano unapopata nafasi ya Kupiga Krosi basi ipigwe kwa wakati, leo namuona Juma Abdul akianza kuliko Hassan Kessy, Ila kama kocha ataingia Kutafuta Sare basi Kessy anaweza kuanza HUKU nafasi ya Ulinzi wa Kushoto Gadiel Michael akiwa na nafasi kubwa ya Kuanza.

Mabeki wa Kati : Kwa Kikosi kilichopo ni wazi Andrew Vicent Dante atasimama na Abdallah Shaibu Ninja ambaye amekuwa moja ya walinzi Muhimu kwenye mechi kadhaa zilizopita kabla ya kuwekwa benchi kwenye mechi dhidi ya Simba.

Viungo wa kati : Namba sita Said Juma Makapu ambaye amekuwa anapocheza namba 6 anasaidia zaidi eneo la Ulinzi na hasa ukizingatia Ugenini inabidi Ujilinde zaidi na Kutafuta nafasi chache ambazo utapata matokeo, Namba 8 Pius Buswita.

Viungo wa Pembeni : Namba 7 Yusuph Mhilu ambaye anakasi kubwa, amekuwa kwenye Kiwango bora siku za karibuni lakini pia anaonekana kucheza akiwa na kiu ya mafanikio , Namba 11 Emmanuel martin.

Washambuliaji : Kutokana na Yanga kuwakosa wachezaji wake wengi waandamizi kama Obrey Chirwa,Ngoma, Tambwe leo Itabidi wacheze watu ambao siyo asili yao kucheza katika nafasi ya Ushambuliaji.

Juma Mahadhi na Raphael Daudi   msomaji wa kalambonews.com
ndiyo wananafasi Kubwa ya Kuanza kama washambuliaji, Lakini benchi laufundi linaweza kumwamini Yohanna Mkomola Kuanza kama mshambuliaji licha ya kuwa nafasi yake inakuwa ngumu kutokana na Kukosa kucheza mechi nyingi za Ligi na hata kimataifa ila kwa leo anaweza kucheza kutokana na Ufinyu wa kikosi.

No comments:

Post a Comment