TUMUSIFU BWANA

prop

Friday, 18 May 2018

Kikosi bora cha vpl kwa wachezaji wa ndani Tanzania

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.

Kikosi bora cha Msimu VPL wachezaji wa Ndani

Kulingana na Ufatiliaji wa karibu wa Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara VPL Kwataunit.com inakuletea Kikosi chake Bora cha Msimu kwa wachezaji wa Ndani (Wale ambao ni Watanzania)

Hii ni Kulingana na Kwataunit na Siyo mawazo au maoni ya mtu mwingine.

> Habari za michezo <

Mfumo ni 4 – 4 – 2

Aishi Manula (Simba) , Amekuwa na Msimu mzuri msimu Huu akiiongoza Simba kupata matokeo katika mechi nyingi huku akiwa ni moja ya Makipa wenye cleansheet nyingi.

Hassan Kessy(Yanga) : Licha ya kuwa na Upinzani kwenye klabu yake upinzani toka kwa mchezaji bora wa VPL msimu wa Mwaka juzi Juma Abdul, Hassan Kessy amekuwa kwenye Kiwango bora msimu Huu

Uwezo wa Kucheza kwa Kujiamini, Kasi ya Kupandisha mashambulizi na kukaba kwa Nguvu na Akili pia kunanifanya nione ni beki wa Kulia Bora msimu Huu.

Gadiel Michael(Yanga) : Kwa wachezaji wa Ndani huyu naye ni moja ya namba 3 waliocheza mechi nyingi ndani ya Klabu ya Yanga na kwa mafanikio makubwa, Gadiel amekuwa mzuri zaidi kwenye Kukaba.

Erasto Nyoni(Simba) : Huyu ni kiraka nimewahi kusikia akisema amewahi kucheza mpaka nafasi ya Kipa akiwa mdogo kwenye  bora cha msimu wachezaji wa ndani Kikosi cha Kwataunit namweka kama namba 4.

Kelvin Yondani(Yanga): Ukizungumza mabeki ambao wamekuwa mhimili mkubwa kwenye Kikosi cha yanga Kelvin Yondani amekuwa muhimu sana, lakini Pia ameonyesha Kiwango bora sana, Kwenye Kikosi changu namweka Namba 5.

Jonas Mkude (Simba): Licha ya kuwa hakuuanza msimu kwa Kupata nafasi lakini amekuwa na kiwango bora sana na Nikuibie siri Katika mechi kadhaa ambazo Mkude alikosekana raundi ya Pili Simba ilitoa sare.

Unakumbuka mechi dhidi ya Mwadui Fc kule Shinyanga? na Ile ya Simba dhidi ya Lipuli kule Iringa?

Shiza Kichuya(Simba) : Moja kati ya wachezaji ambao wanapokuwa Uwanjani wamekuwa katika Kiwango Bora, Huyu anaongoza kwa Assist nyingi kwenye Ligi.

Mudathir Yahya Abbas(Stand United) : Moja ya Viungo watulivu lakini pia wabunifu wanapokuwa uwanjani, Kwenye Kikosi cha Kwataunit namweka kama namba 8 akicheza kati na Jonas Mkude.

John Bocco(Simba) : Amekuwa sumu sana kutokana na aina ya Magoli yake kuwa katika mazingira ya kila namna, Anafaa kuanza kama namba 9 kwenye Kikosi changu.

Marcel Boniventure (Maji Maji): Uwezo Mkubwa wa Kupiga Mashuti ya mbali ni kitu pekee nachompendea Marcel Boniventure licha ya kuwa katika klabu ambayo hapati sana msaada lakini ndiye mchezaji anayewafata Bocco na Okwi akiwa na Magoli 13 nyuma goli moja kwa Bocco mwenye 14.

Sixtus Sabilo(Stand United)  : Moja kati ya wachezaji ambao baadhi ya watu watajiuliza ni nani? Huyu ni moja kati ya wachezaji waliosababisha Stand United ionekane imebadilika sana mzunguko wa Pili, Ndiye mchezaji mwenye magoli mengi Stand United licha ya Kutokea Pembeni kama namba 11.

Anacheza kwa kasi lakini amekuwa mtulivu sana anapokuwa karibu na Lango, Anafaa kuwa kwenye Kikosi cha Kwanza.

Wachezaji wa Akiba

1.Aron Kalambo (Tanzania Prisons)

2.David Luhende (Mwadui Fc)

3.Shomari Kapombe (Simba)

4.Ali Ali (Stand United)

5.Ibrahim Ajibu (Yanga)

6.Himid Mao Mkami (Azam Fc)

7.Adam Salamba (Lipuli Fc)

No comments:

Post a Comment