Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Nyota wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi ‘L0a Pulga’ ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya soka ya Hispania ‘La Liga’, kwa mwezi Aprili.
Messi ambaye anaongoza kwa mabao kwenye ligi hiyo msimu huu ametangazwa mshindi leo Mei 18, 2018 asubuhi na bodi ya La Liga.
Katika mwezi Aprili, Messi amecheza Mechi 4 na kufunga mabao 6 huku akipiga ‘hat-trick’ mbili dhidi ya Leganes na Deportivo La Coruna ambazo zilimfanya kuongeza idadi ya mabao akimwacha hasimu wake, nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
Aprili, Barca imeshinda bao 3-1 dhidi ya Leganes, 2-1 dhidi ya Valencia, sare ya 2-2 dhidi ya Celta Vigo na 4-2 dhidi ya Deportivo La Coruna, mechi ambayo iliwahakikishia ubingwa wa La Liga msimu wa huu.
Messi atakabidhiwa tuzo hiyo kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya Real Sociedad kwenye Uwanja wa Camp Nou. Mechi hiyo ni ya mwisho kwa La Liga msimu huu ambapo Barcelona watamuaga nahodha wao Andres Iniesta ambaye anamalizia msimu na kuondoka Klabuni hapo.
18
May
2018
Next
Newer Post
prop
Friday, 18 May 2018
Mess achukua tunzo ya mchezaji bora wa spain
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment