Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Matokeo Stand United vs Mtibwa Sugar 20 April 2018 Azam Sports
Matokeo ya Moja kwa Moja kati ya Stand United vs Mtibwa Sugar nusu fainali ya Kwanza Azam Sports Federation Cup katika uwanja wa KAMBARAGE SHINYANGA
Mechi Imeanza katika uwanja wa Kambarage Shinyanga
Stand United 0 – 0 Mtibwa Sugar
Dakika ya pili Mtibwa wanapata mpira wa adhabu unapigwa na Kutoka Nje Bado ni 0 kwa 0
Dakika ya 10
Stand United 0 – 0 Mtibwa Sugar
Dakika kumi na Mbili za Mwanzoni Stand United wanaonekana Kucheza Vizuri zaidi ya Mtibwa
Dakika ya 13 Salum Kihimbwa anajaribu shuti la Mbali Kipa wa Stand Anadaka
Dakika ya 13 Stand Wanapata Kona, Kona inakosa Madhara.
Stand United 0 – 0 Mtibwa Sugar
Dakika 20
Stand United 0 – 0 Mtibwa Sugar
Dakika 25 zimekatika katika uwanja wa Kambarage matokeo yakiwa 0 kwa 0
Goaaaaaaaal Hassan Dilunga anaipatia Mtibwa Bao la Kwanza Dilunga kafanya Dribbling akaingia ndani kidogo ya 18 na Kupiga Shuti linaloingia na Kutikisa Nyavu
Dakika 30′
Stand United 0 – 1 Mtibwa Sugar
Dakika ya 38 Hassan Dilunga kwa mara Nyingine anawafunga Stand United
Dakika ya 43 Salum Kihimbwa anaonekana kusumbua mabeki wa Stand United
Stand United 0 – 2 Mtibwa Sugar
Dakika mbili za Nyongeza zimeongezwa kabla ya Kipindi cha Kwanza Kukamilika
HALF TIME
Stand United 0 – 2 Mtibwa Sugar (Magoli ya Hassan Dilunga)
KIPINDI CHA PILI
Kwataunit.com Tunaendelea Kukujuza Kipindi hiki cha Pili
Inapigwa Kona ambayo inakosa madhara kwenye lango la Stand United.
Dakika ya 47 Kipa wa Stand Anafanyiwa mabadiliko Muhonge anatoka anaingia kipa Mwingine Makaka, Anatokea kwenye eneo ambalo siyo rasmi washabiki wanamzomea
Dakika ya 53 Bigirimana Blaise anajaribu Shuti linatoka Nje kwenye lango la Mtibwa Sugar
Dakika ya 58 Stand United wanafanya moja ya jaribio zuri, Almanusra wapate Bao, Zinatokea Piga Nikupige lakini mwisho wa siku wanashindwa kupata Bao
Dakika ya 63 Mtibwa wanapata kona
Inapigwa kona Ndefu mlinzi wa Stand anaondoa mpira kATIKA hatari.
Dakika ya 65 Stand nao wanapata Kona lakini inakosa madhara.
Stand 0 – 2 Mtibwa (30′ , 38′ Hassan Dilunga)
Dakika ya 73 Kelvin Sabato Kiduku anakosa nafasi ya Wazi kwa Mtibwa
Dakika 85
Stand United 0 – 2 Mtibwa
Zimeongezwa dakika 4 za Nyongeza Matokeo yakiwa bado 0 kwa Stand United na 2 kwa Mtibwa Sugar
MPIRA UMEKWISHA
Stand United 0 – 2 Mtibwa Sugar (Magoli yote ya Hassan Dilunga)
Mtibwa Sugar wanafuzu kwenda Fainali ya Azam Sports Federation Cup
prop
Friday, 20 April 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment