TUMUSIFU BWANA

prop

Friday, 20 April 2018

HABARI ZA IVI PUNDE MASOGANGE ATUNAYE TENA DUNIANI.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Video queen maarufu nchini, Agnes Gerald ‘Masogange’ amefariki dunia hivi punde (leo Aprili 20, 2018) katika Kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada kuzidiwa ghafla jana na kukimbizwa hospitalini hapo.

Mwili wa marehemu ukiwekwa kwenye gari kupelekwa Muhimbili kuhifadhiwa.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinadai Masogange alifikishwa Hospitalini hapo akisumbuliwa na homa ya matumbo na tatizo la kupungukiwa na damu. Global Publishers imefika hospitalini hapo na kujionea umati wa watu waliokusanyika wakilia kwa uchungu kumpoteza msanii huyo.

Dkt. Kihama Ngoma ameithibitishia  na kusema taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Tayari mwili wa marehemu Masogange umehaimshwa hospitalini hapo na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, AMEN!.

No comments:

Post a Comment