Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Wakristo ulimwenguni kote wanasheherekea Ijumaa Kuu, wakikumbuka kusulubiwa kwa Yesu na Ijumaa huko Jerusalem, ibada maalum ya pasaka ilifanyika ikifuata utamaduni wa kale katika ardhi hiyo takatifu.
Mahujaji kutoka ulimwenguni kote walifurika Ijumaa katika maeneo mbalimbali kupitia njia finyu zilizoko eneo la Cobblestone wakipitia eneo la Dolorosa katika mji wa zamani wa Jerusalem ili kushiriki katika maandamano ya sherehe za Ijumaa Kuu.
Wamekuwa wakiimba nyimbo za kiroho na kusoma baadhi ya vifungu vya Bibilia, wakifuatilia nyao za Yesu hadi kufika katika vituo 14 vya msalabani.
“Bila shaka niheshima kubwa kwangu kuwa katika ardhi hii tukufu kwa maadhimisho haya. Ni kitu kikubwa sana. Inanisaidia katika imani yangu, inanisaidia katika kila kitu,” amesema Gary Osterberg anaetokea Canada.
Katika ardhi hiyo takatifu, dini na siasa havigawanyiki. Sikukuu ya Pasaka imekuja wiki sita kabla ya mpango wa Marekani kuhamisha ubalozi wake huko Israel kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.
“Nafikiri kuwa kuhamisha kwa ubalozi wa Marekani kwenda Jerusalem ni jambo sahihi. Nafikiri ni kitu muwafaka kufanyika. Na natamani kama Canada ingefuata hilo na kutekeleza uhamisho huo; kuhamisha Ubalozi wa Canada kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.
Lakini Wapalestina wamekasirishwa na hatua hiyo ya kuhamisha ubalozi na uamuzi wa Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kama makao makuu ya Israel. Imad, muuza duka katika soko la Arab bazaar, amesema anatarajia siku za usoni kuwaJerusalem itakuwamji mkuu wa Palestina
“Sitarajii kitu chochote kutoka kwa Donald Trump, bali vitu vibaya. Hili, unafahamu, ni sehemu ya yale ambayo wanayafanya dhidi ya Wapalestina: hatua nyingine, kitu kingine, ambacho kitawaumiza Wapalestina.”
prop
Saturday, 31 March 2018
Wakristo ulimwenguni kote wanatarajia kusherekea paasaka
Recommended Articles
- Habari
LIVE: Abdul Nondo anazungumza na waandishi wa habariJun 10, 2018
BOFYA HAPA KUSIKIA MAONGEZO LIVE SASA
- Habari
HIVI APA VYUO 20 VILIVYOFUNGIWA NA NECTA NA SABABU ZA KUFUNGIWA Jun 08, 2018
Vifahamu vyuo 20 vilivyofungiwa na NACTE na sababu za kufungiwa Leo June 8, 2018 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limefuta usajili...
- Habari
SHUHUDI LIVE MSANII ANAYE TAMBULISHWA NA DK . SHIKAJun 08, 2018
Dk. Shika akimtambulisha msanii wake Mzee maarufu mtandaoni, Dk. Shika ameamua kutumbukia kwenye kiwanda cha Bongo Flava. Leo amemtambulish...
- Habari
Walichoandika wolper,Snura Prof.Jay kuhusu kifo cha samu wa UkweliJun 06, 2018
Walichoandika Wolper, Snura na Prof. Jay kuhusu kifo cha Sam wa Ukweli Usiku wa June 6, 2018 Muimbaji Sam wa Ukweli amefariki dunia baada ya ...
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment