TUMUSIFU BWANA

prop

Sunday, 18 March 2018

Shinyanga ,mwanamke anyongwa mpaka kufa na watu wasio julikana

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
 kwamujibu wa reporter wetu tukio hilo limetokea 17 mwezihuu 
Shinyanga. Watu wasiojulikana wamemnyonga hadi kufa Salome Paschal (30) mkazi wa Kijiji cha Zunzuli katika Kitongoji cha Kituli, Kata ya Salawe wilayani Shinyanga na kisha kuutupa mwili wake kwenye kichaka.

Akizungumza leo Jumapili Machi 18, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, polisi wanaendelea kufanya uchunguzi kwa aliyehusika na mauaji ya hayo.

Akisimulia tukio hilo, mume wa Salome aitwaye Isaya Mshomari amesema mkewe ameuawa Machi 17, 2018 saa nane mchana kwa maelezo kuwa alimuaga kuwa anakwenda sokoni kununua mahitaji ya nyumbani kisha aje awapikie wafanyakazi waliokuwa shambani.

No comments:

Post a Comment