TUMUSIFU BWANA

prop

Thursday 15 March 2018

KAURI YA OKWI KWA WAPINZANI WAO AL MASRY

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.

Mshambuliaji Mganda anayekipiga katika kikosi cha Simba Sc, Emmanuel Okwi, amesema kuwa wameenda Misri kupambana na hawana hofu yoyote kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Al Masry utakaofanyika Jumamosi ya March 17 mwaka huu  huko Misri..

Okwi ameongeza kuwa anaamini Simba ina nafasi kubwa ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na wanachohitaji ni kuwa na bahati tu.

Okwi amesema kuwa uwezo wa kushinda mechi hiyo wanao lakini wanatakiwa kuongeza umakini na kutoziweka akilini "fitna" zozote za nje ya uwanja ambazo zitajitokeza kabla ya kushuka uwanjani.

"Tunakwenda kupambana, naamini Mungu atatusaidia, uwezo tunao, mliwaona, wanafungika," alisema kwa kifupi Mganda huyo.

Katika mchezo wa awali uliofanyika March 7 mwaka huu Jijini Dar es salaam, timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2.

Kutokana na matokeo hayo Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya magoli 3-3 ili iweze kusonga mbele


KWA HABARI ZAIDI PAKUA APP YA KALAMBONEWS KUPATA HABARI ZOTE

No comments:

Post a Comment