Meneja wa Chelsea Antonio Conte
amesema alihisi kwamba kichapo cha 3-0 ambacho klabu yake ilipokezwa
katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano "hakikuwa cha haki".
Lionel
Messi alifunga mabao mawili naye Ousmane Dembele akafunga moja - bao
lake la kwanza akichezea Barca - na kuwasaidia miamba hao wa Uhispania
kuondoka na ushindi wa jumla wa 4-1.Mechi ya kwanza uwanjani Stamford Bridge ilikuwa imemalizika 1-1.
Matokeo hayo yaliwaondoa Chelsea kutoka kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu na msimu ujao wanakabiliwa na kibarua cha kufuzu kutokana na ushindani mkali kwenye nafasi nne za kwanza Ligi ya Premia.
"Hatuna majuto," alisema Conte.
"Ukiitazama mechi hiyo, utaona kwamba matokeo hayo hayakuwa ya haki."
Conte alikiri kwamba Messi - aliyefunga pia bao la Barca mechi ya kwanza Stamford Bridge - ndiye aliyekuwa mwamuzi wa nani mbabe kati ya timu hizo mbili.
Bao la pili la mshambuliaji huyo wa Argentina uwanjani Nou Camp lilifikisha 100, idadi ya mabao ambayo ameyafunga Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO NA BURUDANI, VICHEKESHO PAMOJA NA HABARI MBALIMBALI ZA KITAIFA NA KIMATAIFA PAKUA APP YA KALAMBONEWS KUPITIA PLAY STORE
No comments:
Post a Comment