Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tanga, kimeanza mkakati wa kuhakikisha inalirejesha Jimbo la Tanga Mjini pamoja na kata zake 15, zilizochukuliwa na Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Akizungumza wakati akipokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani juzi katika eneo la Kata ya Duga, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanga, Bakari Mkoba amesema chama hicho kinajivunia kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Mkoba amesema anafanya mikutano ya ndani kuzungumza na wana-CCM katika ziara ya kushukuru kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana na kupokea kero kutoka kwa wananchi.
“Wananchi wengi kwenye ziara yangu ya kushukuru, wanampongeza Rais (John Magufuli) kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuijenga Tanzania mpya... Wapo wapinzani wanarejea CCM kwa vile wanaridhishwa na kazi anayofanya Rais," amesema.
Mkoba aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuitendea haki sekta ya elimu, afya na sekta nyingine ambazo zimeleta mafanikio makubwa ikiwemo kutolewa Sh bilioni 1.4 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa maabara wa vituo vya afya vya Ngamiani, Makorora na Mikanjuni.
Amesema katika kata hiyo, jumla ya wanachama 40 walijiunga na chama hicho na wengine 68 walijiunga kutoka Kata ya Nguvumali na kufanya idadi yao kufikia 108 katika siku ya kwanza ya ziara yake katika kata hizo.
Jimbo la Tanga Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, mgombea Mussa Mbarouk wa CUF alishinda dhidi ya Omari Nundu wa CCM huku chama hicho kikishinda kata 15 za udiwani na CCM ikiambulia kata 12. Hata hivyo, katika Baraza la Halmashauri ya Jiji, Meya ametoka CCM.
prop
Friday, 23 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment