TUMUSIFU BWANA

prop

Saturday, 2 June 2018

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA JUMAMOSI YA 2.2018

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.


Ajenti wa kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen anadai kuwa vilabu kadhaa vina hamu ya kumsaini mchezaji huyo wa Denmark . (London Evening Standard)
Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Christiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 anataka kuichezea Manchester United na atakubali kurudi Old Trafford, kulingana na kocha wa zamani wa Uingereza na Real Madrid Fabio Capello. (Goal.com)


Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Christiano Ronaldo
John Terry anatarajiwa kuunganishwa tena na mchezaji mwenza wa Uingereza na Chelsea Frank Lampard katika klabu ya Derby, baada ya Lampard kuajiriwa kama mkufunzi wa kikosi hicho cha ligi hiyo ya mabingwa. Beki Terry, 37, alitoka Aston Villa baada ya klabu hiyo kushindwa kufuzu katika ligi ya Uingereza ya Premier League. (Star)
Mchezaji wa Liverpool na Ujerumani Emre Can, 24, amekubali kandarasi ya miaka minne na klabu ya Juventus na atafanyiwa ukaguzi wa matibabu na mabingwa hao wa Itali.(Calciomercato)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kukutana na mamake Ousmane Dembele
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kukutana na mamake Ousmane Dembele katika juhudi za kumshawishi mchezaji huyo wa Barcelona na Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 kuhamia Anfield msimu huu. (Mundo Deportivo - in Spanish)

BBC ;source

No comments:

Post a Comment