TUMUSIFU BWANA

prop

Monday 21 May 2018

TETESI ZA SOKA BALANI UKAYA JUMATATU YA 21.2018

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Manchester City
Manchester city wanampango wa kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard,27, kwa mkataba wa £100m baada ya meneja Pep Guardiola kumuweka mchezaji huyo kuwa kiungo muhimu anayemlenga wakati wa uhamisho.(Star)
Klabu ya Utaliano ya AC Milan imempatia kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini,30, mkataba wa miaka mitatu huku kiungo huyo raia wa Ubelgiji kuwa huru kwa uhamisho wa bure katika majira ya joto. (Times - subscription required)
Conte: Nitamsalimia Mourinho kwa mkono
Beki wa Tottenham,Toby Alderweireld, 29, ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuuzwa na klabu ya United wakati wa uhamisho wa majira ya joto. (Mirror)
West Ham inaamini kumteuwa Manuel Pellegrini kama meneja wao mpya wiki hii- ambayo itaipatia nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati Yaya Toure, 35, aliyeiaga Manchester City. (Telegraph)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anatarajiwa kuiaga Chelsea kwa saa 48 zijazo - huku meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo. (Express)

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere
Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 26 yuko tayari kutia saini mkataba wa miaka mitatu aliyopewa na Arsenal , licha ya kupata mapendekezo bora kutoka Everton na Wolves. (Mirror)

Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment