Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Golikipa wa Njombe Mji David Kissu amejibu maswali mengi ambayo yamekuwa yakiibuka kuhusu taulo lake ambalo hulitumia anapokuwa golini wakati wa mechi mbalimbali.
Leo wakati wa mchezo kati ya Njombe Mji dhidi ya Simba alikuwa na taulo lakini dakika ya 17 akafungwa goli goli. Wakati wa mapumziko mwamuzi wa pembeni alimwambia Kissu aliondoe taulo golini.
Baada ya kulitoa taulo golini mashabiki wa Simba wakaenda kulichukua jambo ambalo lilisababisha vurugu zilizopelekea baadhi ya mashabiki kukamatwa na jeshi la polisi.
David Kissu amesema anashangaa kwa nini timu nyingi ambazo zimeenda kucheza uwanja wa Sabasaba zimekuwa zikiamini taulo lake ni tatizo golini.
“Mimi siamini kama taulo linaweza kuzuia goli, taulo ni kwa ajili ya matumizi yangu binafsi. Hata ukiangalia katika mchezo wa leo Aishi Manula alikuwa na taulo lakini langu ndio limeonekana linazuia goli.”
“Kipindi cha kwanza wametufunga 1-0 lakini bado wanakimbia na taulo langu, kama taulo lingekuwa linazuia magoli saizi tungekuwa tunaongoza ligi.”
prop
Tuesday 3 April 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment