Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Wakati siku zikiwa zinazidi kusogea mbele kulekea pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga katika Ligi Kuu Bara msimu huu, kiungo wa Simba, Jonas Mkude, anaamini kikosi chao kitafanya vizuri dhidi ya Yanga baada ya kuondoka kwa Kocha George Lwandamina.
Mkude ambaye ametoka kuwa majeruhi hivi karibuni amesema kuondoka kwa Lwandamina ni pigo kwa Yanga kutokana na namna alivyokuwa msaada mkubwa wa kikosi chao.
Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Mkude ameeleza kuwa kurejea kwa Lwandamina Zesco United itachangiwa kuwaathiri wachezaji wa Yanga kisaikolojia na akisema wanaweza kurejesha kipigo cha mabao 5-0 walichokitoa kwa Yanga msimu wa 2011/12.
“Lwandamina alikuwa ni bonge la kocha ambaye kila mtu aliona mchango wake kwa Yanga, kama ameondoka kweli hilo ni pigo kubwa kwao.
“Lakini pia ni jambo zuri kwetu kwa sababu linaweza kutusaidia tukarudia kuandika rekodi yetu ya msimu wa 2011/12 ambapo tuliifunga Yanga mabao 5-0 tulipokuwa na kikosi bora kama kilivyo hiki cha sasa ambapo kulikuwa wakali kama Emmanuel Okwi, marehemu Patrick Mafisango, Felix Sunzu, Haruna Moshi ‘Boban’, Kelvin Yondani na wengine wengi,” alisema Mkude.
prop
Saturday, 14 April 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment