TUMUSIFU BWANA

prop

Saturday 31 March 2018

Meneja wa mbunge wa arusha lema ahamia ccm

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Katibu Mwenezi wa CHADEMA ambaye pia alikuwa Meneja Kampeni wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Gabrieli Kivuyo (kushoto).
Katibu Mwenezi wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia alikuwa Meneja Kampeni wa Mbunge wa Ausha Mjini, Godbless Lema, Gabrieli Kivuyo jana alikihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai ni utovu wa nidhamu ndani ya CHADEMA.

Aidha, amedai kuwa viongozi wake ikiwemo Mbunge kuwadharau pamoja na kitendo cha kutolewa nje kwenye kikao cha Mameya kwa tuhuma za kuwarekodi.

Akizungumza wakati akipokelewa na Katibu wa CCM-Wilaya, Musa Matotoka, amesema hata akipata matatizo na kumtafuta Mbunge amekuwa hapatiwi ushirikiano.

No comments:

Post a Comment