Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Kikosi cha Simba Kinachoweza kuanza dhidi ya Al Masry leo 17 March 2018
Kulingana na wachezaji walioenda nchini Misri na mazoezi ambayo yamefanyika siku za mwisho mwisho kuelekea pambano kati ya Al Masry na Simba mtandao wa kwataunit.com tunakupa Kikosi cha Utabiri kinachoweza Kuanza leo.
Golini : Aishi Manula bado ni kipa anayeaminiwa na ataendelea kuaminiwa kutokana na uwezo wake kuonekana bado kuwa mzuri lakini pia Uzoefu na mechi za kimataifa inaweza kuwa faida nyingine kulinganisha Said Mohammed Nduda.
Mabeki wa pembeni: Kuna uwezekano mkubwa wa Kuendelea kuwatumia Nicolas Gyan na Asante kwasi kama beki wa Kulia na Beki wa Kushoto kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita.
Mabeki wa Kati : Hakuna Shaka juu ya Nafasi ya mchezaji kiraka Erasto Nyoni kwenye eneo la beki wa Kati na bila shaka kwa Leo ataanza huku nafasi ya beki Mwingine wa Kati atacheza kati ya Mlipili au Juuko Murshid lakini kwa Leo nafasi ya Juuko Murshid ni kubwa zaidi kuanza na Erasto Nyoni.
Viungo wa kati na pembeni: Hii ni nafasi nyingine kwa Wachezaji Jonas Mkude ambaye ni wazi kuwa ni fundi katika eneo la kati, Nafasi nyingine itakuwa kwa Shomari Kapombe ambaye alichezeshwa eneo la kati katika mchezo uliopita na hata mazoezi ya mwisho kabla ya timu kusafiri alionekana kucheza eneo hilo mazoezini.
Wengine msomaji wa kwataunit.com ni Shiza Kichuya na James Kotei, Kotei akicheza kama namba 7 anaweza kusaidia eneo la katikati ya uwanja ambalo imekuwa kawaida kwa Simba kulitawala wakati Shiza Kichuya akitokea kama mchezaji Huru uwanjani kama ambavyo amekuwa akicheza siku za Karibuni akiwa na Kikosi cha Masoud Djuma na kocha Mkuu Pierre Lechantre.
Au kunaweza kukawa na Option ya kumwanzisha Kapombe kama namba 2 na eneo la kati kubadilika kwa kucheza Mkude, Kichuya, Kotei na Said Ndemla ambaye anaweza kusaidia kupiga pasi ndefu au kucheza mipira ya adhabu inayotokea uwanjani au hata kucheza mipira ya mashuti ya Kushtukiza ambayo Ndemla ni mzuri.
Washambuliaji : Katika eneo ambalo linatazamwa zaidi na washabiki wengi wa Simba ni eneo lao la Ushambuliaji kwani wanahitaji magoli zaidi ili kujihakikishia kupeta ni wazi Mganda Emmanuel Okwi ataanza kama Namba kumi akicheza na Nahodha John Raphael Bocco ambaye amekuwa mhimili mkubwa mbele.
prop
Saturday, 17 March 2018
Hikiapa kikosi cha simba vs al masry leo
Recommended Articles
- Michezo
Julio: Alikiba Anaweza Kucheza hata Ulaya Jun 10, 2018
KOCHA wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameweka wazi kuwa msaÂnii wa Bongo Fleva nchini, Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’...
- Michezo
MAMBO MATANO MAKUBWA WALIO HAFIKIANA YANGA SC MKUTANO MKUUJun 10, 2018
Club ya Dar es Salaam Young Africans leo Jumapili ya June 10 2018 ilifanya mkutano mkuu na wanachama wake katika ukumbi wa Police Officers Mess M...
- Michezo
GOR MAHIA WAIPA KICHAPO SIMBA SC...SAFARI YA ULAYA NDO BASI TENAJun 10, 2018
Moja kati ya siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Bongo ni leo June 10 2018, kwani ndio ilikuwa siku inayochezwa mchezo wa...
- Michezo
MATOKEO GOR MAHIA VS SIMBA SC 2_0 KIPINDI CHAPILIJun 10, 2018
Matokeo Gor Mahia vs Simba leo 10 June 2018 Sportpesa Matokeo Gor Mahia vs Simba leo 10 June 2018 Sportpesa Matokeo Gor Mahia vs Simba leo 10 Ju...
Newer Article
Zuma mahakamani kesi ya rushwa
Older Article
Kitazame kikosi cha yanga klabu bingwa afrika
Labels:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment