Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
ULIMWENGU AREJEA AFRIKA NA KUJIUNGA NA WAKONGWE WA SUDAN
Mshambuliaji Thomas Ulimwengu ameamua kurejea barani Afrika na kujiunga na klabu kongwe ya Sudan ya Al Hilal.
Ulimwengu ambaye hucheza nafasi ya ushambuliaji na wakati mwingine winga, nafasi hizo zote ndani ya timu hiyo zina watu wa maana ambapo mmoja anatoka Nigeria na mwingine Brazil.
Mbrazili, Geovane Maranhao, anacheza namba tisa kwenye kikosi hicho, huku Mnigeria, Azeez Shobola akicheza winga, hivyo Ulimwengu anatakiwa kufanya juhudi kubwa kuhakikisha anakuwepo kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Meneja wa Ulimwengu, Jamal Kisongo, alisema kuwa tayari mchezaji huyo amepata timu lakini hawezi kuweka wazi mpaka pale vibali vitakapokamilika.
Straika huyo tayari anaonekana katika mtandao wa Transfer Market, ambao unaonyesha kuwa amesajiliwa na klabu ya Al Hilal, ingawa thamani yake imeshuka tofauti na alivyokuwa na TP Mazembe.
Ulimwengu mara ya mwisho alisajiliwa na klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden akitokea kwenye klabu ya TP Mazembe ya Congo, lakini alishindwa kucheza kutokana na kuandamwa na majeraha ya goti ambayo yamemuweka nje kwa muda mrefu.
Hata hivyo ikiwa inaaminika kuwa alisaini wikiendi iliyopita, Championi jana lilimtafuta Ulimwengu kwa muda mrefu lakini hakupatikana, juhudi zinaendelea.
prop
Thursday, 24 May 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment