TUMUSIFU BWANA

prop

Monday, 7 May 2018

TETESI ZA USAJILI SIMBA JUMANNE YA 8.2018

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Tetesi za Usajili Simba leo 8 May 2018

Ukiongelea moja kati ya wachezaji nyota nchini kwasasa lazima utamtaja Shiza Ramadhan Kichuya kutokana na Ubora alionao ndani ya Ligi Kuu.

Kichuya hafungi sana kama ilivyokuwa katika msimu uliopita lakini msimu Huu anafunga na Kutoa pasi nyingi za mabao kiasi cha kuwa ndiye mchezaji anayeongoza kwa pasi za usaidizi (Assist).

Mkataba wa Simba na Shiza Ramadhan Kichuya unamalizika mwishoni mwa Msimu huu na baada ya hapo Kichuya atakuwa mchezaji Huru na timu yoyote Ile inaweza kufanya naye mazungumzo na kumalizana naye.

Mpaka sasa Kichuya anahusishwa kutua katika Klabu ya Tp Mazembe ya nchini Congo moja kati ya Timu zinazofanya vizuri katika michuano ya Kimataifa karibu kila Mwaka.

Mwenyewe Alonga Msimamo wake baada ya Mkataba

Kichuya msomaji wa Kwataunit.com ameweka wazi kuwa baada ya mkataba timu ya Kwanza anayotaka kuipa nafasi ya Kuongea nayo ni klabu yake ya Simba ndipo atasikiliza ofa kutoka kwa timu nyingine nje ya Simba.

Pesa Anayoitaka ili Aongeze mkataba.

Shiza Kichuya alisema ili Aongeze mkataba Simba au kusaini kwenye timu nyingine basi ni lazima dau lake liwe mara tatu zaidi ya lile dau alilosajiliwa wakati anatoka Mtibwa Sugar kujiunga na Simba.

Kichuya alisajiliwa kwa dau la Milioni 20 hivyo kwasasa zinatakiwa milioni 60 ndipo asaini.

No comments:

Post a Comment