TUMUSIFU BWANA

prop

Sunday, 6 May 2018

MCHEZAJI WA SIMBA : AJIBU NA CHILWA NI WASALITI

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Baada ya nyota saba wa Yanga wakiwemo Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa kushindwa kuondoka na timu hiyo kwenda Algeria, straika wa zamani wa Simba na Yanga, Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’, amesema wachezaji hao na wenzao ni wasaliti.


Nyota hao ‘waligoma’ lakini kwa aina yake wakitoa udhuru kila mtu kwa mtindo wake lakini nyuma ya pazia ikielezwa wanagoma wakishinikiza walipwe malimbikizo ya mishahara yao.

Yanga Alhamis ya wiki jana kwenda Algeria kushiriki mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi USM Alger mechi ya Kundi D

Wachezaji ambao hawakuondokaondoka na timu ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshishimbi, Ibrahin Ajibu, Thabani Kamusoko na Beno Kakolanya.

Mogella alisema kuwa wachezaji hao ni wasaliti kwani walipaswa kutanguliza maslahi ya nchi halafu mambo mengine yangefuata baadaye.

“Klabu zinapaswa kuwa makini kutimiza mahitaji ya wachezaji hao kama walikubaliana jambo fulani liwe hivi basi watekeleze na si vinginevyo kama haya yanayotokea kwa Yanga.

“Lakini wachezaji wa Yanga nao ni wasaliti sababu walitakiwa kutanguliza mbele maslahi ya klabu kwanza ukiangalia wachezaji ambao hawajaondoka na timu ni wale ambao ni tegemeo,” alisema Mogella.

Naye straika wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ alisema: “Wachezaji wa sasa wanatakiwa kubadilika sababu wamekuwa wakitanguliza maslahi mbele kuliko kazi kama ilivyokuwa zamani.” alisema.

Hata hivyo Yanga imeshindwa kutamba mbele ya USM Alger kwa kukubali kufungwa jumla ya mabao 4-0, mchezo ukipigwa dimba la Julai 5 1962 Jumapili ya jana.

Chanzo: Championi

No comments:

Post a Comment