TUMUSIFU BWANA

prop

Sunday, 6 May 2018

Matokeo ya mchezo wa USM ALGER VS YANGA SC HAYA APA

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Matokeo Shirikisho : USM Alger vs Yanga 6.5.2018

Matokeo Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF hatua ya makundi kati ya wenyeji USM Alger  dhidi ya Yanga , Mechi inachezwa katika uwanja wa  ” Stade du 5 Julliet ” huko Algeria

Kuanzia saa 4 Kamili Usiku Tutakupa Matokeo moja kwa Moja.

Mechi Imeanza

USM Alger 0 – 0 Yanga

Dakika ya 2 Faulo kuelekea Yanga, Inapigwa Dante anaokoa kwa Kichwa

Dakika ya 4 USM Alger wanapata bao kupitia kwa Oussama Darfalou

USM Alger 1 – 0 Yanga

Dakika ya 7 USM Alger wanaonekana kucheza kwa Kasi wakati Yanga wakilinda zaidi

Dakika ya 9 USM Alger wanapata kona, Yanga wanaokoa kwa kichwa

Dakika 12 Zimekatika, USM Alger wanaonekana kutumia zaidi mawinga wanaopiga Krosi katikati hata Goli lao limepatikana kwa Style Hiyo.

Dakika ya 13 Mahadhi anaondoka anapiga Mpira lakini mabeki wa Alger wanaokoa

USM Alger 1 – 0 Yanga

Dakika ya 16 Darfalou anawakosa tena Yanga goli anapiga Mpira Unapaa

Dakika 20

USM Alger 1 – 0 Yanga

Dakika ya 22 USM Alger wanapata kona nyingine, Lakini walinzi wa Yanga wanakuwa makini kuokoa.

Dakika ya 25 Yanga wanapata Kona, Inapigwa na Mahadhi lakini Abdallah Shaibu Ninja anaonekana kucheza Faulo kabla ya Kuruka Kuucheza mpira

DAKIKA 30

USM Alger 1 – 0 Yanga

Dakika ya 31 Inapigwa FreE kick kuelekea Yanga Rostand Anaokoa inakuwa Kona.

Dakika ya 32 kona Iliyopigwa inazaa Goli kwa USM Alger

USM Alger 2 – 0 Yanga

Dakika 40

USM Alger 2 – 0 Yanga

Dakika ya 43 Yanga wanapata Mpira wa Adhabu Unapigwa kipa anatema lakini hakuna Mtu wa Kumalizia kazi, Mabeki wa Alger wanaokoa

HALF TIME

USM Alger 2 – 0 Yanga

KIPINDI CHA PILI

Ngoma Inaendelea Kuchezwa hapa

Dakika ya 46

USM Alger 2 – 0 Yanga

Dakika ya 50 Dante anaonekana Kupata Mushkeli anatibiwa na Kuambiwa Atoke Nje kisha arejee uwanjani.

Dakika ya 53 USM Alger wanapata bao la 3

USM Alger 3 – 0 Yanga

DAKIKA 60 Rostand anaokoa goli jingine lilikuwa la Nne hili

Dakika ya 61 Raphael Daud anatoka anaingia Juma Abdul

Dakika ya 63 Juma Mahadhi anapewa kadi ya Njano kwa Mchezo usio wa Kiungwana

DAKIKA 70

USM Alger 3 – 0 Yanga

Dakika ya 77 Yusuph Mhilu anatoka anaingia Yohanna Mkomola

Dakika ya 82 Said Juma makapu anapewa kadi ya Njano

USM Alger 3 – 0 Yanga

Dakika ya 85 Said Juma Makapu anatoka nafasi yake inachukuliwa na Pato Ngonyani

Dakika 2 Za Nyongeza

Refa anawapa Penati USM ALger, Penati inapigwa na Kipa wa Alger goaaaaal

FULL TIME

USM Alger 4 – 0 Yanga

No comments:

Post a Comment