TUMUSIFU BWANA

prop

Tuesday 29 May 2018

DK JPM AKIWA NA KATIBU MPYA WA CCM

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
 STORIES BREAKING: Huyu ndie Katibu Mkuu Mpya wa CCM Taifa


Leo May 29, 2018 Dkt. Bashiru Ali Kakurwa ndiye aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu Mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo alipendekezwa na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini DSM.

Hii ni baada ya Aliyekuwa Katibu Mkuu Kinana kuomba kujiuzulu na kukubaliwa na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa.

Imethibitishwa katika taarifa ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) iliyoketi tarehe 28-29 May 2018 Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Bashiru Ally alikuwa Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na Rais Magufuli kufanya Uhakiki wa mali za Chama cha Mapinduzi CCM.

No comments:

Post a Comment